Hakuna sekta ulimwenguni inayotoa fursa za kazi mbalimbali kama usimamizi wa Biashara. Siku hizi, nafasi za kazi za biashara na usimamizi zimehama kutoka makampuni na mahoteli/migahawa peke yake. Usimamizi wa biashara na taasisi za huduma zinahitaji watu wenye ujuzi zaidi katika maswala ya usimamizi; watu wenye ujuzi wanahitajika katika biashara za kuandaa matukio; makampuni makubwa yanahitaji wataalamu zaidi; wageni katika ndege na wateja wa mabenki wanahitaji huduma bora zaidi; na wataalamu vijana wanatafuta fursa ya kutekeleza mawazo yao ya kibiashara.
OUS inatoa kozi mbalimbali za kila aina, zikiwemo za kusoma kutoka nyumbani au masomo ya muda. Ili kuwapa motisha wanafunzi, tunatumia njia za kisasa na za ubunifu kufundisha. Wanafunzi wanawasiliana mara kwa mara na waalimu na kupokea msaada wa kibinafsi wanapouhitaji.
Wanaosomea shahada ya kwanza, ya pili au udaktari katika taalumu yoyote wanahitaji viwango kamili. OUS ni chuo kilichoidhinishwa na kina vibali kutoka taasisi zinazosimamia elimu mbali mbali zikiwemo inje na ndani ya Uswisi. Vyama hivi na vibali hivi ndivyo huhakikisha kiwango cha juu cha elimu kinachotoka hapa. Wafanyakazi wa OUS wanatoa huduma ya viwango vya juu kwa wanafunzi wetu.
Sio jambo la ajabu kwamba watu wana imani katika huduma zetu: Hakuna maandalizi bora zaidi katika sekta ya biashara na usalama yenye mazoezi ya vitendo , masomo ya muda na yenye kufundisha katika lugha ya kiingereza.
Kila mwaka, wanafunzi wengi kutoka nchi nyingi ulimwenguni hupanga maisha yao ya baadaye ya kitaalamu kupitia masomo haya.
Mazingira ya kimataifa yanawezesha wanafunzi wetu kuelewa desturi na tamaduni tofauti wakati wa mafunzo yao na huwawezesha kuunda mitandano ambayo ni muhimu kwa ajili ya kazi zao ya baadae.